Isaiah 28:21
Bwana atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu, 2 ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni: 1 ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu, 2 ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 29:21Bwana atamtwaa peke yake kutoka makabila ya Israeli kwa maangamizo, kulingana na laana zote za Agano zilizoandikwa kwenye Kitabu hiki cha Sheria.
Joshua 10:11Walipokuwa wakikimbia mbele ya Israeli kwenye barabara iteremkayo kutoka Beth-Horoni hadi Azeka, Bwana akawavumishia mawe makubwa ya mvua kutoka mbinguni, na wengi wao wakauawa na hayo mawe kuliko wale waliouawa kwa upanga wa Waisraeli.
2 Samuel 5:20Ndipo Daudi akaenda mpaka Baal-Perasimu, na huko akawashinda Wafilisti. Akasema, “Kama mafuriko yafurikavyo, Bwana amewafurikia adui zangu mbele yangu.” Kwa hiyo mahali hapo pakaitwa Baal-Perasimu. + 5:20 Maana yake Bwana Afurikae.
1 Chronicles 14:11Hivyo Daudi pamoja na watu wake wakakwea mpaka Baal-Perasimu, + 14:11 Maana yake ni Bwana Afurikae. akawashinda huko. Akasema, “Kama maji yafurikavyo, Mungu amewafurikia adui zangu kwa kutumia mkono wangu.” Kwa hiyo mahali pale pakaitwa Baal-Perasimu.
Isaiah 10:12Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.”
Isaiah 29:14Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa, 2 kwa ajabu juu ya ajabu. 1 Hekima ya wenye hekima itapotea, 2 nayo akili ya wenye akili itatoweka.” 1