Isaiah 38:19
Walio hai, walio hai: hao wanakusifu, 2 kama ninavyofanya leo. 1 Baba huwaambia watoto wao 2 habari za uaminifu wako. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 18:19Kwa maana nimemchagua yeye, ili awaongoze watoto wake na jamaa yake kufuata njia ya Bwana, kwa kuwa waadilifu na kutenda haki, ili Bwana atimize ahadi yake kwa Abrahamu.”
Exodus 12:26Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’
Deuteronomy 4:9Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.
Deuteronomy 6:7Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo.
Joshua 4:21Akawaambia Waisraeli, “Wazao wenu watakapowauliza baba zao siku zijazo wakisema, ‘Mawe haya maana yake ni nini?’
Psalms 78:4Hatutayaficha kwa watoto wao; 2 tutakiambia kizazi kijacho 1 matendo yastahiliyo sifa ya Bwana, 2 uweza wake, na maajabu aliyoyafanya. 1