Isaya 47:9
Haya mawili yatakupata, kufumba na kufumbua, 2 katika siku moja: 2 kufiwa na watoto, na ujane. 1 Yote yatakupata kwa kipimo kikamilifu, 2 ijapokuwa uchawi wako ni mwingi, 2 na uaguzi wako ni mwingi. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Ruth 1:20Akawaambia, “Msiniite tena Naomi, + 1:20 Naomi maana yake Wa Kupendeza, Wa Kufurahisha. niiteni Mara, + 1:20 Mara maana yake Chungu. kwa sababu Mwenyezi + 1:20 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. amenitendea mambo machungu sana.
Isaiah 13:18Mishale yao itawaangusha vijana, 2 hawatakuwa na huruma kwa watoto wachanga 2 wala hawataangalia watoto kwa huruma. 1
Isaiah 47:12“Endelea basi na uaguzi wako, 2 na wingi wa uchawi wako, 2 ambao umeutumikia tangu utoto wako. 1 Labda utafanikiwa, 2 labda unaweza ukasababisha hofu kuu. 1
Jeremiah 51:29Nchi inatetemeka na kugaagaa, 2 kwa kuwa makusudi ya Bwana dhidi ya Babeli yanasimama: 1 yaani, kuangamiza nchi ya Babeli 2 ili pasiwe na yeyote atakayeishi humo. 1
Daniel 2:2Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme,
Daniel 5:7Mfalme akawaita wasihiri, wanajimu na waganga waletwe, naye akawaambia hawa wenye hekima wa Babeli, “Yeyote asomaye maandishi haya na kuniambia maana yake atavikwa nguo za zambarau, na kuvikwa mkufu wa dhahabu shingoni mwake, naye atafanywa mtawala wa cheo cha tatu katika ufalme.”