Isaiah 49:18
Inua macho yako ukatazame pande zote: 2 wana wako wote wanakusanyika na kukujia. 1 Kwa hakika kama vile niishivyo, 2 utawavaa wote kama mapambo, 1 na kujifunga nao kama bibi arusi,” 2 asema Bwana. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
17Wana wako wanaharakisha kurudi, 2 nao wale waliokuteka wanaondoka kwako. 1
Cross References
Genesis 13:14Baada ya Loti kuondoka Bwana akamwambia Abramu, “Ukiwa hapo ulipo, inua macho yako utazame kaskazini na kusini, mashariki na magharibi.
Proverbs 17:6Wana wa wana ni taji la wazee, 2 nao wazazi ni fahari ya watoto wao. 1
Isaiah 45:23Nimeapa kwa nafsi yangu, 2 kinywa changu kimenena katika uadilifu wote 2 neno ambalo halitatanguka: 1 Kila goti litapigwa mbele zangu, 2 kwangu mimi kila ulimi utaapa. 1
Isaiah 49:22Hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: 1 “Tazama, nitawaashiria watu wa Mataifa, 2 nitainua bendera yangu kwa mataifa; 1 watawaleta wana wako mikononi yao, 2 na kuwabeba binti zenu juu ya mabega yao. 1
Isaiah 54:1“Imba, ewe mwanamke tasa, 2 wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto; 1 paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha, 2 wewe ambaye kamwe hukupata utungu; 1 kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi 2 kuliko wa mwanamke mwenye mume,” 4 asema Bwana. 1
Isaiah 54:9“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa, 2 nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia. 1 Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi, 2 kamwe sitawakemea tena. 1