Isaya 52:5
“Basi sasa nina nini hapa?” asema Bwana. 1 “Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo, 2 nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,” 4 asema Bwana. 1 “Mchana kutwa 2 jina langu limetukanwa bila kikomo. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 1:13kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili.
Exodus 3:7Bwana akamwambia, “Hakika nimeona mateso ya watu wangu katika Misri. Nimesikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao, nami naguswa na mateso yao.
Psalms 44:12Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, 2 wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao. 1
Psalms 74:10Ee Mungu, mtesi atakudhihaki mpaka lini? 2 Je, adui watalitukana jina lako milele? 1
Psalms 74:22Inuka, Ee Mungu, ujitetee; 2 kumbuka jinsi wapumbavu 2 wanavyokudhihaki mchana kutwa. 1
Isaiah 22:16Unafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa 2 kujikatia kaburi lako mwenyewe, 1 ukichonga kaburi lako mahali palipo juu, 2 na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba? 1