Isaya 54:10
Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe, 2 hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, 1 wala agano langu la amani halitaondolewa,” 2 asema Bwana, mwenye huruma juu yenu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Psalms 46:2Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa 2 nayo milima ikiangukia moyoni mwa bahari. 1
Psalms 89:33lakini sitauondoa upendo wangu kwake, 2 wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe. 1
Isaiah 49:15“Je, mama aweza kumsahau mtoto 2 aliyeko matitini mwake akinyonya, 1 wala asiwe na huruma 2 juu ya mtoto aliyemzaa? 1 Ingawa anaweza kusahau, 2 mimi sitakusahau wewe! 1
Isaiah 54:8Katika ukali wa hasira 2 nilikuficha uso wangu kwa kitambo, 1 lakini kwa fadhili za milele 2 nitakuwa na huruma juu yako,” 2 asema Bwana Mkombozi wako. 1
Isaiah 61:8“Kwa maana Mimi, Bwana, napenda haki, 2 na ninachukia unyangʼanyi na uovu. 1 Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao 2 na kufanya agano la milele nao. 1
Malachi 2:5“Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu.