Yeremia 2:25
Usikimbie hadi miguu yako iwe haina viatu, 2 na koo lako liwe limekauka. 1 Lakini ulisema, ‘Haina maana! 2 Ninaipenda miungu ya kigeni, 2 nami lazima niifuatie.’ 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Deuteronomy 28:48kwa hiyo katika njaa na kiu, katika uchi na umaskini wa kutisha, utawatumikia adui ambao Bwana atawatuma dhidi yako. Yeye ataweka nira ya chuma shingoni mwako hadi amekwisha kukuangamiza.
Deuteronomy 32:16Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni, 2 na kumkasirisha kwa sanamu zao 2 za machukizo. 1
2 Chronicles 28:23Akatoa kafara kwa miungu ya Dameski, waliokuwa wamemshinda, kwa kuwa aliwaza, “Kwa kuwa miungu ya mfalme wa Aramu imewasaidia wao, nitaitolea dhabihu ili inisaidie na mimi.” Lakini haya ndiyo yaliyokuwa maangamizi yake na Israeli wote.
Isaiah 20:2wakati ule Bwana alisema kwa kinywa cha Isaya mwana wa Amozi. Akamwambia, “Vua nguo ya gunia kutoka mwilini mwako na viatu kutoka miguuni mwako.” Naye akafanya hivyo, akatembea huku na huko uchi, bila viatu.
Jeremiah 3:13Ungama dhambi zako tu: 2 kwamba umemwasi Bwana Mungu wako, 1 umetapanya wema wako kwa miungu ya kigeni 2 chini ya kila mti unaotanda, 2 nawe hukunitii mimi,’ ” 4 asema Bwana.
Jeremiah 14:10Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu hawa: 1 “Wanapenda sana kutangatanga, 2 hawaizuii miguu yao. 1 Hivyo Bwana hawakubali; 2 sasa ataukumbuka uovu wao 2 na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.”