Jeremiah 46:21
Askari wake waliokodiwa katika safu zake 2 wako kama ndama walionenepeshwa. 1 Wao pia watageuka na kukimbia pamoja, 2 hawataweza kuhimili vita, 1 kwa maana siku ya msiba inakuja juu yao, 2 wakati wao wa kuadhibiwa. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
20“Misri ni mtamba mzuri, 2 lakini kipanga anakuja dhidi yake kutoka kaskazini. 1
Cross References
Deuteronomy 32:15Yeshuruni + 32:15 Yeshuruni maana yake ni Yeye aliye mnyofu, yaani Israeli (ona pia Kum 33:26; Isa 44:2 ). alinenepa na kupiga teke; 2 alikuwa na chakula tele, 2 akawa mzito na akapendeza sana. 1 Akamwacha Mungu aliyemuumba, 2 na kumkataa Mwamba Mwokozi wake. 1
2 Kings 7:6kwa kuwa Bwana alilifanya jeshi la Waaramu lisikie sauti kama ya magari ya vita, farasi na jeshi kubwa, kiasi kwamba waliambiana, “Tazama, mfalme wa Israeli ameajiri mfalme wa Wahiti na mfalme wa Wamisri kuja kutushambulia sisi!”
Proverbs 15:17Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo 2 kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki. 1
Isaiah 34:7Nyati wataanguka pamoja nao, 2 ndama waume na mafahali wakubwa. 1 Nchi yao italowana kwa damu, 2 nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama. 1
Jeremiah 46:5Je, ninaona nini? 2 Wametiwa hofu, 1 wanarudi nyuma, 2 askari wao wameshindwa. 1 Wanakimbia kwa haraka 2 pasipo kutazama nyuma, 2 tena kuna hofu kuu kila upande,” 4 asema Bwana. 1
Jeremiah 46:15Kwa nini mashujaa wako wamesombwa 2 na kupelekwa mbali? 1 Hawawezi kusimama, kwa maana Bwana 2 atawasukuma awaangushe chini. 1