Leviticus 19:32
“ ‘Uwapo mbele ya mzee, simama ili kuonyesha heshima kwa wazee, nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
33“ ‘Wakati mgeni anaishi pamoja nawe katika nchi yako, usimnyanyase.
Cross References
Genesis 48:12Ndipo Yosefu akawaondoa wanawe magotini mwa Israeli naye akasujudu hadi nchi.
1 Kings 2:19Bathsheba alipokwenda kwa Mfalme Solomoni kuzungumza naye kwa ajili ya Adoniya, mfalme alisimama kumlaki mama yake, akamwinamia na kuketi kwenye kiti chake cha ufalme. Akaamuru kiti cha ufalme kuletwa kwa ajili ya mama yake mfalme, naye akaketi mkono wake wa kuume.
Job 32:6Basi Elihu mwana wa Barakeli wa kabila la Buzi akasema: 1 “Mimi ni mdogo kwa umri, 2 nanyi ni wazee; 1 ndiyo sababu niliogopa, 2 sikuthubutu kuwaambia kile ninachojua. 1
Proverbs 20:29Utukufu wa vijana ni nguvu zao, 2 mvi ni fahari ya uzee. 1
Lamentations 5:12Wakuu wametungikwa juu kwa mikono yao, 2 wazee hawapewi heshima. 1
1 Timothy 5:1Usimkemee mzee kwa ukali bali umshawishi kama vile angekuwa ni baba yako. Uwatendee vijana kama vile ndugu zako;