Proverbs 14:2
Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana, 2 bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
1 Kings 3:6Solomoni akajibu, “Umemfanyia mtumishi wako, baba yangu Daudi, fadhili nyingi, kwa kuwa alikuwa mwaminifu kwako na mwenye haki, tena mnyofu wa moyo. Nawe umemzidishia fadhili hii kuu kwani umempa mwana wa kuketi kwenye kiti chake cha ufalme, kama ilivyo leo.
Job 1:1Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.
Job 28:28Naye Mungu akamwambia mwanadamu, 2 ‘Kumcha Bwana: hiyo ndiyo hekima, 2 nako kujitenga na uovu ndio ufahamu.’ ”
Psalms 112:1Msifuni Bwana. 1 Heri mtu yule amchaye Bwana, 2 mtu yule apendezwaye sana na amri zake. 1
Proverbs 2:15ambao mapito yao yamepotoka 2 na ambao ni wapotovu katika njia zao. 1
Proverbs 16:6Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; 2 kwa kumcha Bwana mtu hujiepusha na ubaya. 1