Proverbs 30:17
“Jicho lile limdhihakilo baba, 2 lile linalodharau kumtii mama, 1 litangʼolewa na kunguru wa bondeni, 2 litaliwa na tai. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
16Ni kaburi, tumbo lisilozaa, 2 nchi isiyoshiba maji kamwe, 2 na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ 1
18“Kuna vitu vitatu vinavyonishangaza sana, 2 naam, vinne nisivyovielewa: 1
Cross References
Genesis 9:21Alipokunywa huo mvinyo wake akalewa na akalala uchi kwenye hema lake.
Deuteronomy 21:18Kama mtu ana mwana mkaidi na mwasi ambaye hamtii baba yake na mama yake, na hasikii wazazi wanapomrudi,
Deuteronomy 28:26Mizoga yenu itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa nchi, wala hapatakuwepo mtu yeyote wa kuwafukuza.
2 Samuel 18:9Basi ikawa Absalomu alikutana na watu wa Daudi. Yeye alikuwa amepanda nyumbu wake, naye nyumbu alipopita chini ya matawi yaliyosongana ya mwaloni mkubwa, kichwa cha Absalomu kilinaswa kwenye mti. Akaachwa akiningʼinia hewani, wakati nyumbu aliyekuwa amempanda aliendelea kwenda.
2 Samuel 21:10Rispa binti Aiya akachukua nguo ya gunia, akajitandikia juu ya mwamba. Kuanzia mwanzo wa mavuno mpaka mvua ziliponyesha juu ya miili ya hao waliouawa, Rispa hakuruhusu ndege wa angani kuwagusa wakati wa mchana, wala wanyama wa mwitu wakati wa usiku.
Proverbs 23:22Msikilize baba yako, aliyekuzaa, 2 wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee. 1