Kumbukumbu 33:17
Katika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza; 2 pembe zake ni pembe za nyati, 1 na kwa pembe hizo atapiga mataifa, 2 hata yaliyo miisho ya dunia. 1 Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu; 2 hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 48:19Lakini baba yake akakataa, akasema, “Ninajua, mwanangu, ninajua. Yeye pia atakuwa taifa, naye pia atakuwa mkuu. Hata hivyo, ndugu yake mdogo atakuwa mkuu kuliko yeye, nao wazao wake watakuwa kundi la mataifa.”
Numbers 24:8“Mungu alimleta kutoka Misri; 2 yeye ana nguvu kama nyati. 1 Anayararua mataifa yaliyo adui zake, 2 na kuvunja mifupa yao vipande vipande; 2 huwachoma kwa mishale yake. 1
Numbers 26:37Hizi ndizo zilizokuwa koo za Efraimu; wale waliohesabiwa walikuwa 32,500. Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yosefu kwa koo zao.
Joshua 17:18bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”
1 Chronicles 5:1Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa.
1 Chronicles 5:23Idadi ya nusu ya kabila la Manase walikuwa wengi sana, Wakakaa kuanzia Bashani hadi Baal-Hermoni, yaani mpaka Seniri na mlima Hermoni.