Genesis 49:3
“Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, 2 nguvu zangu, tunda la kwanza la nguvu zangu, 2 umepita kwa heshima, umepita kwa uwezo. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
2“Kusanyikeni na msikilize, enyi wana wa Yakobo, 2 msikilizeni baba yenu Israeli. 1
Cross References
Genesis 35:22Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili. Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili: 1
Genesis 46:8Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri: 1 Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. 1
Numbers 1:20Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli: 2 Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
Deuteronomy 21:17Ni lazima amkubali mwana wa mke asiyempenda kama mzaliwa wa kwanza kwa kumpa sehemu ya vile vyote alivyo navyo maradufu. Mwana huyo ni ishara ya kwanza ya nguvu za baba yake. Haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye. 1 Mwana Mwasi
Deuteronomy 33:6“Reubeni na aishi, asife, 2 wala watu wake wasiwe wachache.”
1 Chronicles 5:1Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli (yeye alikuwa mzaliwa wa kwanza, lakini kwa kuwa alikinajisi kitanda cha baba yake, haki zake za mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yosefu mwana wa Israeli. Hivyo hakuorodheshwa kwenye orodha ya ukoo wao kulingana na haki yake ya kuzaliwa.