Hagai 1:6
Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.”
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
5Sasa hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu.
7Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Zitafakarini vyema njia zenu.
Cross References
Leviticus 26:26Nitakapowaondolea upatikanaji wa mkate wenu, wanawake kumi wataoka mkate wenu katika tanuru moja, nao wataugawa mkate kidogo kwa kupima. Mtakula, lakini hamtashiba.
Deuteronomy 28:38Utapanda mbegu nyingi katika shamba lakini utavuna haba, kwa sababu nzige watazila.
1 Kings 17:12Akamjibu, “Hakika kama Bwana Mungu wako aishivyo, sina mkate wowote, isipokuwa konzi ya unga kwenye gudulia na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili kwamba tule, kiishe, tukafe.”
Job 20:28Mafuriko yataichukua nyumba yake, 2 maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu. 1
Proverbs 11:24Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi, 2 mwingine huzuia, lakini huwa maskini. 1
Jeremiah 12:13Watapanda ngano lakini watavuna miiba; 2 watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote. 1 Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako 2 kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.”