Hosea 9:13
Nimemwona Efraimu, kama Tiro, 2 aliyeoteshwa mahali pazuri. 1 Lakini Efraimu wataleta 2 watoto wao kwa mchinjaji.” 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
12Hata wakilea watoto, 2 nitamuua kila mmoja. 1 Ole wao 2 nitakapowapiga kisogo! 1
14Wape, Ee Bwana, 2 je, utawapa nini? 1 Wape matumbo ya kuharibu mimba 2 na matiti yaliyokauka. 1
Cross References
Job 27:14Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, 2 fungu lao ni kuuawa kwa upanga; 1 wazao wake hawatakuwa kamwe 2 na chakula cha kuwatosha. 1
Lamentations 2:22“Kama ulivyoita siku ya karamu, 2 ndivyo ulivyoagiza hofu kuu 2 dhidi yangu kila upande. 1 Katika siku ya hasira ya Bwana 2 hakuna yeyote aliyekwepa au kupona; 1 wale niliowatunza na kuwalea, 2 adui yangu amewaangamiza.”
Ezekiel 27:3Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: 1 “ ‘Ee Tiro, wewe umesema, 2 “Mimi ni mkamilifu katika uzuri.” 1
Hosea 10:14mngurumo wa vita utainuka dhidi ya watu wako, 2 ili kwamba ngome zako zote zitaharibiwa: 1 kama Shalmani alivyoharibu Beth-Arbeli katika siku ile ya vita, 2 wakati mama pamoja na watoto wao 2 walipotupwa kwa nguvu ardhini. 1
Hosea 13:16Watu wa Samaria ni lazima wabebe hatia yao, 2 kwa sababu wameasi dhidi ya Mungu wao. 1 Wataanguka kwa upanga; 2 watoto wao wadogo watatupwa kwa nguvu ardhini, 2 wanawake wao walio na mimba watatumbuliwa.”
Amos 7:17“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana: 1 “ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini, 2 nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga. 1 Shamba lako litapimwa na kugawanywa, 2 na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani. 1 Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni, 2 mbali na nchi yao.’ ”