Isaiah 3:8
Yerusalemu inapepesuka, 2 Yuda inaanguka; 1 maneno yao na matendo yao ni kinyume na Bwana, 2 wakiudharau uwepo wake uliotukuka. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
2 Chronicles 28:5Kwa hiyo Bwana Mungu wake akamtia mikononi mwa mfalme wa Aramu. Waaramu wakamshinda, wakachukua watu wake wengi mateka na kuwaleta mpaka Dameski. Tena alitiwa mikononi mwa mfalme wa Israeli, ambaye aliwaua watu wake wengi.
2 Chronicles 33:6Akawatoa wanawe kuwa kafara kwa kuwapitisha katika moto katika Bonde la Ben-Hinomu, akafanya ulozi, uaguzi na uchawi, akataka ushauri kwa wenye pepo wa utambuzi na wenye kuwasiliana na mizimu. Akafanya maovu mengi machoni pa Bwana, akaichochea hasira yake.
2 Chronicles 36:17Mungu akamwinua dhidi yao mfalme wa Wakaldayo, aliyewaua vijana wao wa kiume kwa upanga ndani ya mahali patakatifu, ambaye hakumbakiza kijana mwanaume wala kijana mwanamke, wazee wala vikongwe. Mungu akawatia wote mikononi mwa Nebukadneza.
Proverbs 26:27Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, 2 kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia. 1
Isaiah 5:18Ole wao wanaovuta dhambi kwa kamba za udanganyifu 2 na uovu kama kwa kamba za mkokoteni, 1
Isaiah 57:4Mnamdhihaki nani? 2 Ni nani mnayemcheka kwa dharau, 2 na kumtolea ndimi zenu? 2 Je, ninyi si watoto wa waasi, 2 uzao wa waongo? 1