Isaiah 31:8
“Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu; 2 upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza. 1 Watakimbia mbele ya upanga 2 na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Genesis 49:15Aonapo palivyo pazuri mahali pake pa kupumzika 2 na jinsi nchi yake inavyopendeza, 1 atainamisha bega lake kwenye mzigo 2 na kujitolea kwa ajili ya kazi ngumu. 1
2 Chronicles 32:21Naye Bwana akamtuma malaika ambaye aliangamiza wanajeshi wote, na viongozi na maafisa katika kambi ya mfalme wa Ashuru. Kwa hiyo, mfalme wa Ashuru akarudi nchini mwake kwa aibu. Naye alipokwenda katika hekalu la mungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua kwa upanga.
Isaiah 10:16Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 atatuma ugonjwa wa kudhoofisha kwa askari wake walio hodari, 1 katika fahari yake moto utawaka 2 kama mwali wa moto. 1
Isaiah 10:33Tazama, Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, 2 atayakata matawi kwa nguvu kuu. 1 Miti mirefu sana itaangushwa, 2 ile mirefu itashushwa chini. 1
Isaiah 17:13Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi, 2 wakati anapoyakemea yanakimbia mbali, 1 yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima, 2 kama jani livingirishwapo na dhoruba. 1
Isaiah 30:27Tazama, Jina la Bwana linakuja kutoka mbali, 2 likiwa na hasira kali inayowaka 2 pamoja na wingu zito la moshi, 1 midomo yake imejaa ghadhabu 2 na ulimi wake ni moto ulao. 1