Isaiah 61:9
Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa, 2 na uzao wao miongoni mwa kabila za watu. 1 Wale wote watakaowaona watatambua 2 kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.” 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Numbers 22:12Lakini Bwana akamwambia Balaamu, “Usiende pamoja nao. Hupaswi kulaani watu hao, kwa kuwa wamebarikiwa.”
Isaiah 44:3Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu, 2 na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka; 1 nitamimina Roho wangu juu ya watoto wako, 2 nayo baraka yangu juu ya wazao wako. 1
Zechariah 8:13Jinsi mlivyokuwa kitu cha laana katikati ya mataifa, ee Yuda na Israeli, ndivyo nitakavyowaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Msiogope, bali iacheni mikono yenu iwe na nguvu.”
Acts 3:26Mungu alipomfufua Yesu Mwanawe, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki kwa kumgeuza kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya.”
Romans 11:16Kama sehemu ya donge la unga uliotolewa kuwa limbuko ni mtakatifu, basi unga wote ni mtakatifu, nalo shina kama ni takatifu, vivyo hivyo na matawi nayo.