Yeremia 4:7
Simba ametoka nje ya pango lake, 2 mharabu wa mataifa amejipanga. 1 Ametoka mahali pake 2 ili aangamize nchi yenu. 1 Miji yenu itakuwa magofu 2 pasipo mtu wa kuishi humo. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Leviticus 26:31Nitaifanya miji yenu kuwa magofu, na kuharibu mahali patakatifu penu pa kuabudia, nami sitapendezwa na harufu nzuri ya sadaka zenu.
2 Kings 24:1Wakati wa utawala wa Yehoyakimu, Nebukadneza mfalme wa Babeli aliishambulia nchi, naye Yehoyakimu akawa mtumwa wake kwa miaka mitatu. Lakini hatimaye akabadili mawazo yake na kuasi dhidi ya Nebukadneza.
Isaiah 1:7Nchi yenu imekuwa ukiwa, 2 miji yenu imeteketezwa kwa moto; 1 nchi yenu imeachwa tupu na wageni 2 mbele ya macho yenu, 2 imeharibiwa kama vile imepinduliwa na wageni. 1
Isaiah 6:11Ndipo nikasema, “Hadi lini, Ee Bwana?” Naye akanijibu: 1 “Hadi miji iwe imeachwa magofu 2 na bila wakazi, 1 hadi nyumba zitakapobaki bila watu, 2 na mashamba yatakapoharibiwa na kuangamizwa, 1
Jeremiah 5:6Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawashambulia, 2 mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza, 1 chui atawavizia karibu na miji yao, 2 ili kumrarua vipande vipande yeyote atakayethubutu kutoka nje, 1 kwa maana maasi yao ni makubwa, 2 na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi. 1
Jeremiah 9:11“Nitaifanya Yerusalemu lundo la magofu, 2 makao ya mbweha; 1 nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa 2 ili asiwepo atakayeishi humo.”