Mark 4:11
Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa kujua siri ya Ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walioko nje, kila kitu husemwa kwao kwa mifano,
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Matthew 13:11Akawajibu, “Ninyi mmepewa kuzifahamu siri za Ufalme wa Mbinguni, lakini wao hawajapewa.
Matthew 16:17Naye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona, + 16:17 Bar-Yona ni neno la Kiaramu, maana yake ni Mwana wa Yona. kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni.
Luke 10:21Wakati huo Yesu akashangilia katika Roho Mtakatifu, akasema, “Nakuhimidi Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo. Naam, Baba, kwa kuwa hivyo ndivyo ilivyokupendeza.
1 Corinthians 5:12Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kanisa? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani?
Ephesians 1:9Naye alitujulisha siri ya mapenzi yake sawasawa na uradhi wa mapenzi yake, ambayo alikusudia katika Kristo,
Colossians 4:5Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.