Micah 7:4
Aliye mwema kupita wote kati yao 2 ni kama mchongoma, 1 anayeonekana mnyofu zaidi miongoni mwao 2 ni mbaya kuliko uzio wa miiba. 1 Siku ya walinzi wako imewadia, 2 siku atakayokutembelea Mungu. 1 Sasa ni wakati wao 2 wa kuchanganyikiwa. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 10:3Mtafanya nini siku ya kutoa hesabu, 2 wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali? 1 Mtamkimbilia nani awape msaada? 2 Mtaacha wapi mali zenu? 1
Isaiah 55:13Badala ya kichaka cha miiba 2 itaota miti ya misunobari, 1 na badala ya michongoma 2 utaota mhadasi. + 55:13 Mhadasi ni aina ya mti ambao huota milimani karibu na Yerusalemu, hutoa harufu nzuri itumikayo kutengeneza manukato; kwa Kiebrania ni “hadas”, na ilikuwa inatumika kujenga vibanda wakati wa Sikukuu ya Vibanda (ona pia Neh 8:15 ). 1 Hili litakuwa jambo la kumpatia Bwana jina, 2 kwa ajili ya ishara ya milele, 2 ambayo haitaharibiwa.”
Jeremiah 10:15Havifai kitu, ni vitu vya kufanyia mzaha tu, 2 hukumu yavyo itakapowadia, vitaangamia. 1
Ezekiel 12:23Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Nitaikomesha mithali hii, nao hawataitumia tena katika Israeli.’ Waambie, ‘Siku zimekaribia wakati kila maono yatakapotimizwa.
Amos 8:2Akaniuliza, “Amosi, unaona nini?” Nikajibu, “Kikapu chenye matunda yaliyoiva.” Ndipo Bwana akaniambia, “Wakati umewadia kwa watu wangu Israeli; sitawahurumia zaidi.”
Luke 21:25“Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Hapa duniani, mataifa yatakuwa katika dhiki na fadhaa kutokana na ngurumo na misukosuko ya bahari.