Hosea 2:9
“Kwa hiyo nitachukua nafaka yangu wakati itakapokomaa 2 na divai yangu mpya wakati itakapokuwa tayari. 1 Nitamnyangʼanya sufu yangu na kitani yangu 2 iliyokusudiwa kufunika uchi wake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Isaiah 17:10Mmemsahau Mungu Mwokozi wenu, 2 hamkumkumbuka Mwamba aliye ngome yenu. 1 Kwa hiyo, hata ingawa mlipandikiza mimea iliyo mizuri sana 2 na kuotesha mizabibu ya kigeni, 1
Ezekiel 16:39Kisha nitakutia mikononi mwa wapenzi wako, nao watabomoa majukwaa yako na kuharibu mahali pako pa fahari pa ibada ya miungu. Watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vya thamani na kukuacha uchi na bila kitu.
Daniel 11:13Kwa maana mfalme wa Kaskazini atakusanya jeshi jingine kubwa kuliko lile la kwanza; na baada ya miaka kadha, atasonga mbele na jeshi kubwa mno lililoandaliwa vizuri.
Hosea 8:7“Wanapanda upepo 2 na kuvuna upepo wa kisulisuli. 1 Bua halina suke, 2 halitatoa unga. 1 Kama lingetoa nafaka, 2 wageni wangeila yote. 1
Joel 2:14Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma 2 na kuacha baraka nyuma yake: 1 sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji 2 kwa ajili ya Bwana Mungu wenu. 1
Haggai 1:6Mmepanda vingi, lakini mmevuna haba. Mnakula lakini hamshibi, mnakunywa, lakini hamtosheki. Mnavaa nguo, lakini hamsikii joto. Mnapata mishahara, lakini inatoweka kama imewekwa kwenye mfuko uliotobokatoboka.”