Isaya 14:30
Maskini kuliko maskini wote watapata malisho, 2 nao wahitaji watalala salama. 1 Lakini mzizi wako nitauangamiza kwa njaa, 2 nayo njaa itawaua walionusurika. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Job 18:13Nayo yatakula sehemu ya ngozi yake; 2 mzaliwa wa kwanza wa mauti atakula maungo yake. 1
Isaiah 5:17Kondoo watajilisha kwenye malisho yao wenyewe, 2 wana-kondoo watajilisha katika magofu ya matajiri. 1
Isaiah 8:21Watazunguka katika nchi yote, wakiwa na dhiki na njaa. Watakapotaabika kwa njaa, watapatwa na hasira kali, nao, wakiwa wanatazama juu, watamlaani mfalme wao na Mungu wao.
Isaiah 30:23Pia atawapa mvua kwa ajili ya mbegu mnazootesha ardhini, chakula kinachotoka ardhini kitakuwa kizuri sana, tena tele. Katika siku ile, ngʼombe wenu watalisha katika shamba pana la majani.
Isaiah 37:30“Hii ndiyo itakuwa ishara kwako, ee Hezekia: 1 “Mwaka huu utakula kile kiotacho chenyewe, 2 na mwaka wa pili utakula kutoka machipukizi yake. 1 Lakini katika mwaka wa tatu panda na uvune, 2 panda mashamba ya mizabibu na ule matunda yake. 1
Isaiah 65:13Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: 1 “Watumishi wangu watakula, 2 lakini ninyi mtaona njaa; 1 watumishi wangu watakunywa 2 lakini ninyi mtaona kiu; 1 watumishi wangu watafurahi, 2 lakini ninyi mtaona haya. 1