Isaiah 47:14
Hakika wako kama mabua makavu; 2 moto utawateketeza. 1 Hawawezi hata kujiokoa wao wenyewe 2 kutokana na nguvu za mwali wa moto. 1 Hapa hakuna makaa ya kumtia mtu yeyote joto; 2 hapa hakuna moto wa kuota. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 5:12Basi watu wakatawanyika kote nchini Misri kukusanya mabua ya kutumia badala ya nyasi.
Isaiah 5:24Kwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi, 2 na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto, 1 ndivyo mizizi yao itakavyooza 2 na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi; 1 kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote 2 na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli. 1
Isaiah 30:14Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo 2 ukipasuka pasipo huruma 1 ambapo katika vipande vyake 2 hakuna kipande kitakachopatikana 1 kwa kuukulia makaa kutoka jikoni 2 au kuchotea maji kisimani.”
Isaiah 41:2“Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki, 2 akimwita katika haki kwa utumishi wake? 1 Huyatia mataifa mikononi mwake, 2 na kuwatiisha wafalme mbele zake. 1 Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake, 2 huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake. 1
Jeremiah 51:30Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana, 2 wamebaki katika ngome zao. 1 Nguvu zao zimekwisha, 2 wamekuwa kama wanawake. 1 Makazi yake yameteketezwa kwa moto, 2 makomeo ya malango yake yamevunjika. 1
Jeremiah 51:58Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: 1 “Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa, 2 na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto; 1 mataifa yanajichosha bure, 2 taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.”