Isaya 65:25
Mbwa mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, 2 naye simba atakula nyasi kama maksai, 2 lakini mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. 1 Hawatadhuru wala kuharibu 2 katika mlima wangu mtakatifu wote,” 4 asema Bwana.
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
24Kabla hawajaita, nitajibu, 2 nao wakiwa katika kunena, nitasikia. 1
Cross References
Genesis 3:14Hivyo Bwana Mungu akamwambia nyoka, “Kwa kuwa umefanya hili, 1 “Umelaaniwa kuliko wanyama wote 2 wa kufugwa na wa porini! 1 Utatambaa kwa tumbo lako 2 na kula mavumbi 2 siku zote za maisha yako. 1
Isaiah 11:6Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, 2 naye chui atalala pamoja na mbuzi, 1 ndama, mwana simba na ngʼombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja, 2 naye mtoto mdogo atawaongoza. 1
Isaiah 11:9Hawatadhuru wala kuharibu 2 juu ya mlima wangu mtakatifu wote, 1 kwa kuwa dunia itajawa na kumjua Bwana 2 kama maji yajazavyo bahari.
Isaiah 65:11“Bali kwenu ninyi mnaomwacha Bwana 2 na kuusahau mlima wangu mtakatifu, 1 ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati, + 65:11 Bahati alikuwa mungu wa Wakaldayo ambaye pia alijulikana kama Gadi. 2 na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa 2 kwa ajili ya Ajali, + 65:11 Ajali au Meni alikuwa mungu wa majaliwa. 1
Micah 4:3Atahukumu kati ya mataifa mengi, 2 na ataamua migogoro ya mataifa 2 yenye nguvu na yaliyo mbali. 1 Watafua panga zao ziwe majembe, 2 na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. 1 Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, 2 wala hawatajifunza vita tena. 1
Zechariah 8:3Hili ndilo asemalo Bwana: “Nitarudi Sayuni na kufanya makao Yerusalemu. Kisha Yerusalemu utaitwa mji wa kweli, mlima wa Bwana Mwenye Nguvu Zote utaitwa Mlima Mtakatifu.”