Ayubu 26:8
Huyafungia maji kwenye mawingu yake, 2 hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake. 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
He bindeth up the waters in his thick clouds; and the cloud is not rent under them.
In Context
7Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; 2 naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu. 1
9Huufunika uso wa mwezi mpevu, 2 akitandaza mawingu juu yake. 1
Cross References
Genesis 1:7Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo.
Job 37:11Huyasheheneza mawingu kwa maji, 2 naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo. 1
Job 38:37Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? 2 Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni 1
Psalms 135:7Hufanya mawingu kupanda kutoka miisho ya dunia; 2 hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua 2 na huleta upepo kutoka ghala zake. 1
Proverbs 30:4Ni nani ameshapanda mbinguni na kushuka? 2 Ni nani ameshakusanya upepo 2 kwenye vitanga vya mikono yake? 1 Ni nani ameshafungia maji kwenye nguo yake? 2 Ni nani ameimarisha miisho yote ya dunia? 1 Jina lake ni nani, na mwanawe anaitwa nani? 2 Niambie kama unajua! 1
Jeremiah 10:13Atoapo sauti yake, maji yaliyo katika mbingu hunguruma; 2 huyafanya mawingu yainuke kutoka miisho ya dunia. 1 Hupeleka umeme wa radi pamoja na mvua, 2 naye huuleta upepo kutoka ghala zake. 1