Maombolezo 1:9
Uchafu wake umegandamana na nguo zake; 2 hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye. 1 Anguko lake lilikuwa la kushangaza, 2 hapakuwepo na yeyote wa kumfariji. 1 “Tazama, Ee Bwana, teso langu, 2 kwa maana adui ameshinda.” 1
Biblia (Kiswahili)
In The King James Version
In Context
Cross References
Exodus 3:7Bwana akamwambia, “Hakika nimeona mateso ya watu wangu katika Misri. Nimesikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao, nami naguswa na mateso yao.
Exodus 4:31nao wakaamini. Nao waliposikia kuwa Bwana anajishughulisha nao, na kwamba ameona mateso yao, walisujudu na kuabudu.
Deuteronomy 32:27Lakini nilihofia dhihaka za adui, 2 adui asije akashindwa kuelewa, 1 na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; 2 Bwana hakufanya yote haya.’ ” 1
1 Samuel 1:11Naye akaweka nadhiri, akisema, “Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, laiti ungeangalia huzuni kuu ya mtumishi wako na kunikumbuka mimi, wala usimsahau mtumishi wako nawe ukampa mwana, basi huyo mwana nitamtoa kwa Bwana kwa siku zote za maisha yake, wala wembe hautapita kichwani mwake.”
2 Kings 14:26Bwana alikuwa ameona jinsi kila mmoja katika Israeli, awe mtumwa au aliye huru, alivyoteseka kwa uchungu; hapakuwepo na yeyote wa kuwasaidia.
Psalms 25:18Uangalie mateso na shida zangu 2 na uniondolee dhambi zangu zote. 1